Friday, August 17, 2007

Tujinafasi

Karibuni wote wanamtandao kujinafasi katika mambo mseto karne ya ishirini na mbili,

Najua wazi tuna ajenda kem kem za kufundisha , kuliwaza na hata kudadavua,Basi nachukua fursa hii muafaka kuwaomba mjimwage kwa stahaa hasa pale mnapojadili maswala muhimu ya kijamii,itikadi, na ya kiuchumi.Ni vema tukajua kuwa kizazi kijacho katika karne ya ishirini na mbili ni kizazi pevu,kijeuri katika sayansi na teknolojia.Hivyo basi wasije kutuona malimbukeni ya kizazi tulicho.Kwani tukirudi nyuma katika historia inabidi tuwafagilie sana wnwteknolojia wa kizazi kilichopita hasa katika fani tulipo.Kwani tukizungumzia utandawazi katika mawasiliano hakika wametimiza wajibu wao.Uende kona yoyote ya dunia shurti upate mawasilano na upande wa pili wa dunia.Mathalani nchini Tanzania kule vijijini ujumbe mfupi wa simu unaweza kuutuma kutoka kona moja hadi nyingine ya nchi.Hivyo hivyo na mawasiliano ya intaneti.

Ni ukweli usiositirika tukiamini kwamba hakuna mwanzo usiokuwa mgumu na safari ndefu hata iweje inaanza na hatua moja. Nasi basi tuanzie hapa kukishauri kizazi kijacho katika mambo yale muhimu.Tuachane na swala zima la dhima ya maendeleo ya kisiasa,Tujizamishe zaidi namna ambavyo mchango mkubwa wa sayansi na teknojia linavyochangia kubadili kizazi kimoja hadi kingine.Si sahihi sana tukijikita katika maswala magumu ya kufikiria jinsi tunavyoishi sasa na jinsi watakavyishi kizazi kijacho.Haya shime wajemeni fungueni vichwa vyenu kwa kwenda mbele kifikira na kimatendo.

No comments: